Entertainment

Rapa Toxic Lyrikali Akiri Kunusurika Kifo Kufuatia Uvamizi wa Genge la Watu 40.

Rapa Toxic Lyrikali Akiri Kunusurika Kifo Kufuatia Uvamizi wa Genge la Watu 40.

Rapa Toxic Lyrikali amevunja ukimya na kutoa ufafanuzi kuhusu tukio la kikatili lililompata jana usiku katika eneo la Kiamaiko Nairobi ambapo alivamiwa ghafla na watu wasiojulikana.

Kupitia Insta Live, Toxic amethibitisha kutokea kwa uvamizi huo akisema alishambuliwa na genge la watu takriban 40 akiwa na washirika wake watatu. Amesema kuwa licha ya kuzidiwa nguvu na idadi hiyo kubwa ya watu, kwa bahati nzuri walifanikiwa kutoka wakiwa hai.

Picha na video zinazosambaa mtandaoni zinaonyesha gari lake likiwa limevunjwa vioo vyote na kuharibiwa vibaya huku ripoti zikidai kuwa mali za thamani ikiwemo cheni za dhahabu na vifaa vingine viliporwa wakati wa vurugu hizo.

Licha ya Toxic kusisitiza kuwa washirika wa kundi lake la 34 brick wako salama, ripoti ambazo bado hazijathibitishwa zinasambaa kwa kasi zikidai kuwa mmoja wa washirika wake huenda amepoteza maisha kufuatia majeraha ya shambulio hilo. Hata hivyo, rapa huyo hajaweka wazi hali ya majeraha ya wenzake wala kuthibitisha madai hayo ya kifo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *