Entertainment

Eric Omondi Azindua Safari ya Nairobi-Busia kwa Ajili ya Kuchangisha Fedha.

Eric Omondi Azindua Safari ya Nairobi-Busia kwa Ajili ya Kuchangisha Fedha.

Mwanaharakati na mchekeshaji maarufu, Eric Omondi, ameweka wazi azma yake mpya ya kutembea kwa miguu kutoka Nairobi hadi Busia, kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazoendeleza ujenzi wa kituo cha uokozi cha Sisi Kwa Sisi.

Kupitia ujumbe wake kwa umma, Omondi amesema safari hiyo ya siku tano inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 2 Machi mwaka huu. Amesisitiza kuwa hatasimama hadi ndoto ya kukamilisha kituo cha Sisi Kwa Sisi itimie kwa ajili ya wakenya wenye uhitaji.

Hata hivyo mchekeshaji huyo, amewasihi Wakenya watakaokuwa njiani kumpokea na kuendelea kuchangia kile walicho nacho ili kufikia malengo ya mradi huo.

Tangazo hili limekuja ikiwa ni siku chache tu tangu Omondi akamilishe ziara nyingine ya kihistoria ya kutembea kwa miguu kutoka Nairobi hadi Mombasa ambapo alifanikiwa kukusanya mamilioni ya fedha yaliyoelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho cha Sisi Kwa Sisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *