AKOTHEE ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUUGUA GHAFLA

AKOTHEE ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUUGUA GHAFLA

Staa wa muziki ambaye pia ni mfanyabiashara nchini Akothee amelazwa hospitali kwa mara nyingine mara baada ya kuugua ghafla. Akothee ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba alikimbizwa hospitali Disemba 11 alipougua ghafla nyumbani kwake. Hitmaker huyo wa “Sweet Love”  amesema ameshindwa kubaini maradhi yanayomsibu ila kwa sasa ni mwingi wa shukrani kwani ameanza kupata afueni. Bosi huyo wa Akothee Safaris ametambua mchango wa mpenzi wake Nelly Oaks ambaye amesimama nae mara tano hospitali alipokuwa amelazwa hospitalini. Wiki iliyopita binti yake Rue Baby alilazimika kuahirisha hafla ya kufuzu kwake kutoka chuo kikuu baada ya Akothee kulazwa tena hospitalini.

Read More
 AKOTHEE AREJEA TENA KEMPINSIKI BAADA YA KUUSUTA VIKALI UONGOZI WAKE

AKOTHEE AREJEA TENA KEMPINSIKI BAADA YA KUUSUTA VIKALI UONGOZI WAKE

Nyota wa muziki nchini Akothee amerejea tena katika hoteli ya kifahara ya Kempinski,ikiwa ni wiki mbili imepita baada ya kuhapa kutokanyaga kwenye hoteli hiyo. Hatua hiyo ya Akothee imeonekana kuwakera wakenya kwenye mitandao ya kijamii wengi wakisema msanii huyo ni mnafiki na kauli  chafu aliyoitoa juu ya hoteli ya Kempinski haiwezi haribu brand ya hoteli hiyo. Akothee alikuwa anahudhuria hafla ya kusherekea mafanikio ambayo kinara wa ODM Raila Odinga ameiletea taifa la Kenya wikiendi hii iliyopita. Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita Akothee aliichana hoteli ya kifahari ya Kempinski iliyoko jijini Nairobi kwa madai ya kuwa na uongozi mbaya kwani mameneja wa hoteli hiyo walimsumbua sana kipindi anasherekea mwaka mmoja wa kuzinduliwa kwa wakfu wake wa Akothee Foundation katika hoteli hiyo.

Read More