NADIA MUKAMI AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI

NADIA MUKAMI AWACHANA WANAOMKOSOA MTANDAONI

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amewajibu wanaomkosoa kwenye mitandao wa kijamii kutokana na mavazi aliyovalia juzi kati kwenye onesho lake huko Meru. Nadia kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram amesema licha ya watu kukosoa mavazi yake mtandaoni onesho lake huko Meru ilipata mapokezi mazuri, ambapo ameenda mbali na kudai kuwa yeye ni moja kati wanawake ambao huwa hawakati tamaa kirahisi kwa sababu ni mpambanaji. Hitmaker huyo wa ngoma ya Zawadi amesema ataendelea kutia bidii kuhakikisha muziki wake unawafikia wengi kwani anafahamu kwamba wasanii wengi wa kike wamekuwa wakipitia changamoto nyingi kukubalika kwenye tasnia ya muziki nchini haswa baada ya kuwapata watoto katika maisha yao. “Now that I got your attention with the outfit, the event was successful. I am not a woman who gives up, I work hard. It is even harder when you have given birth, and you are a female artist. I alone, understand what I have been going through. It is challenging I have addressed the issues female artistes go through after giving birth.” Ameandika Instagram. Utakumbuka hii sio mara ya kwanza kwa Nadia Mukami kushambuliwa mtandaoni, mwaka wa 2020 watu walimtupia kila aina ya matusi kiasi cha kutangaza kuchukua mapumziko mafupi kwenye mitandao ya kijamii.

Read More
 NADIA MUKAMI AWAPA SOMO VIJANA KUHUSU SAFARI YA UZAZI NA MALEZI

NADIA MUKAMI AWAPA SOMO VIJANA KUHUSU SAFARI YA UZAZI NA MALEZI

Msaniii kike nchini Nadia Mukami amewashauri kwa akina mama wa chang kukubali usaidizi pindi wanapohitaji wakiwa kwenye harakati za kuwalea wanao. Katika kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram na Mashabiki zake Nadia amesema hatua hiyo itasaidia kuondokana na  matatizo ya afya akili yanatokana na malezi ya watoto. Katika hatua nyingine Nadia Mukami ametoa changamoto kwa vijana kujipanga kiuchumi kabla kuwapata watoto kwani majukumu ya malezi sio mapesi kama wengi wanavyodhani. Kauli ya Nadia Mukami inakuja mara baada ya kuweka wazi kuwa ameongeza uzito kutoka kilo 55 hadi 63 kutokana kula chakula kingi kwa ajili ya kupata maziwa ya kumnyonyesha mtoto wake Hasib Kai ambaye ana umri wa miezi miwili.

Read More
 NADIA MUKAMI AFUNGUKA KUHUSU SAFARI YAKE YA KUWA MAMA

NADIA MUKAMI AFUNGUKA KUHUSU SAFARI YAKE YA KUWA MAMA

Msanii nyota nchini Nadia Mukami amefunguka tusiyoyajua kuhusu safari yake ya kumlea na kumnyonyesha mtoto wake wa kiume Hasib Kai ambaye ana umri wa miezi miwili. Katika kikao cha maswali na mashabiki zake kwenye mtandao wa Instagram Nadia Mukami amesema ameongeza uzito kutoka kilo 55 hadi 63 jambo ambalo amedai limechangiwa na yeye kula chakula kingi ili aweze kumnyonyesha mtoto wake bila kizingiti. Mbali na hayo hitmaker huyo wa ngoma ya “Zawadi” ameweka wazi baadhi ya vitu ambavyo alikuwa hapendi alipokuwa  mjazito kwa kusema kwamba hakuwahi vutiwa na nyama ya ngombe, maziwa pamoja na mkate. Hata hivyo kauli ya Nadia Mukami imezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wamempongeza kwa hatua ya kumpa mtoto wake kipau mbele kwenye malezi tofauti na wanawake wengi  ambao hawapendi kuwanyonyesha watoto wao kwa ajili ya kulinda urembo wao.

Read More
 NADIA MUKAMI AFUNGUKA MENGI KUHUSU WAKFU WA LOLA & SAFARI, KUADILI DINI NA MSANII WAKE LATINOH

NADIA MUKAMI AFUNGUKA MENGI KUHUSU WAKFU WA LOLA & SAFARI, KUADILI DINI NA MSANII WAKE LATINOH

Msanii nyota nchini Nadia Mukami amefunguka sehemu ambayo wanapata ufadhili wa wakfu wao Lola na Safari ambao unalenga kuwasaidia wasichana wenye umri mdogo waliopata watoto wakiwa wajanga. Katika mahojiano na Mungai Eve, Nadia amesema wamekuwa wakipata usaidizi kutoka kwa makampuni wanayofanya kazi nao lakini pia kutoka kwa wahisani na marafiki zao huku akitoa wito kwa yeyote anayetaka kutoa msaada wowote kufanya hivyo bila kusita ili waweza kuwasaidia watu wenye uhitaji kwa jamii. Hitmaker huyo wa “Zawadi” amesema wataendelea kurudisha fadhila kwa jamii bila kukoma huku akidokeza ujio wa tovuti ya wakfu wao wa lola na safari ambao waliuzindua kumuenzi mtoto wao aliyefariki mwaka jana kabla hajazaliwa. Mbali na hayo, Nadia amefunguka kuhusu ishu ya kubadili dini kwa kusema bado hajapata shinikizo kutoka kwa mchumba wake arrow boy huku akisisitiza kuwa hana mpango wa kufanya hivyo kwa kuwa upendo ndio dini iliyowaleta pamoja. Kuhusu msanii wake Latinoh, Nadia mukami amesema msanii huyo aliye chini lebo yake ya seven hub creative ataanza kuachia kazi zake mfululizo bila kupoa kama msanii huru hivi karibuni ikizingatiwa kuwa tayari wamefanya ngoma mbili pamoja ambazo Zawadi na Siwezi.

Read More
 NADIA MUKAMI KURUDISHA FADHILA KWA JAMII KUPITIA LOLA & SAFARI FOUNDATION

NADIA MUKAMI KURUDISHA FADHILA KWA JAMII KUPITIA LOLA & SAFARI FOUNDATION

Msanii Nadia Mukami amehamua kurudisha fadhila kwa jamii kupitia wakfu wake wa Lola & Safari. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia Mukami amesema siku ya kina Mama Duniani Mei 8, wakfu wa Lola & Safari umeamua kuandaa hafla ya kuwasherekea kina mama wenye umri mdogo huko jijini Nairobi ambapo watatoa elimu na msaada wa vyakula na mavazi kwao. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Maombi” amesema hakuna mtoto wa kike anapaswa kukatisha ndoto zake kutokana na mimba za mapema kwani kupitia Lola & Safari watafunzwa jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha. Utakumbuka Lola & Safari ni wakfu ambao ulizinduliwa kabla ya Nadia Mukami hajajifungua mtoto wake Hasib Kai na ililenga kusaidia kina mama wenye umri mdogo ambao wametelekezwa na watu wao wa karibu. Wakfu wa “Lola and Safari Foundation” iliyo chini ya Nadia Mukami na Arrow Bwoy tayari imewapatia dili la Ubalozi wa hospitali ya Ruai Family Hospital (RFH)

Read More
 NADIA MUKAMI AACHIA RASMI BUNDLE OF JOY EP

NADIA MUKAMI AACHIA RASMI BUNDLE OF JOY EP

Msanii nyota nchini Nadia Mukami ameachia EP yake mpya ambayo ni zawadi kwa mashabiki zake na shukran kwa mwenyezi Mungu baada ya kujifungua salama. EP hiyo inakwenda kwa jina la Bundle of Joy ina jumla ya nyimbo 4 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Arrow boy, Latinoh na Iyanii. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Nadia Mukami amesema EP hiyo aliitengeneza kipindi yupo na ujauzito wa Mtoto wake wa Kiume haseeb kai huku akidai kwamba aliwekeza moyo wake wote kwenye Bundle of Joy EP. EP hiyo ambayo ina nyimbo kama  Zawadi, Kai wangu, Acheni Mungu aitwe Mungu, na Salute kwa Mama inapatikana kwenye digital platforms mbali mbali za kustream muziki duniani ikiwemo boomplay. Bundle of Joy ni EP ya pili kwa mtu mzima Nadia Mukami ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2020 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo African Pop star iliyokuwa na jumla ya mikwaju 7 ya moto.

Read More
 NADIA MUKAMI KUACHIA EP YAKE MPYA, ALHAMISI HII

NADIA MUKAMI KUACHIA EP YAKE MPYA, ALHAMISI HII

Msanii nyota nchini Nadia Mukami ametangaza kuachia EP mpya chini ya  lebo yake ya muziki ya Seven Hub Creatives ambayo ni zawadi kwa mashabiki zake na shukran kwa mwenyezi Mungu baada ya kujifungua salama. EP hiyo inakwenda kwa jina la Bundle of Joy itakuwa na jumla ya nyimbo 4 ambazo amewashirikisha wakali kama Arrow boy, Latinoh na Iyanii. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Nadia Mukami ameshare artwork pamoja na Tracklist ya EP hiyo ambayo ina nyimbo kama  Zawadi, Kai wang, Acheni Mungu aitwe Mungu, na Salute kwa Mama. Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea Bundle of Joy  EP ambayo itaingia sokoni rasmi Aprili 21 mwaka wa 2022 kupitia mtandao wa Boomplay Kenya huku akitarajia kuachia video ya wimbo wake uitwao Zawadi ambayo amemshirikisha Latinoh siku ya kesho. Hii inaenda kuwa EP ya pili kwa mtu mzima Nadia Mukami ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2020 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo African Pop star iliyokuwa na jumla ya mikwaju 7 ya moto.

Read More
 NADIA MUKAMI AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA ARROW BOY

NADIA MUKAMI AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA ARROW BOY

Msanii nyota nchini Arrow Boy amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake Nadia Mukami ambaye pia ni mwanamuziki. Kwenye performance yao  katika hafla ya uzinduzi wa Focus album Usiku wa kuamkia Machi 13 jijini Nairobi, Arrow Boy alipiga goti na kumvisha Pete Nadia Mukami ambapo alienda mbali zaidi na kuahidi yupo tayari kufunga nae ndoa,  jambo lilomfanya Nadia Mukami amwage machozi ya furaha huku mashabiki wakiwashangilia kwa hatua ya kuanika wazi mahusiano yao. Haya yanajiri ikiwa ni  siku chache baada ya Wawili hao kuweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kwenye uzinduzi wa wakfu wao wa “Lola & Safari” Utakumbuka Mwezi Agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami pamoja na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu.

Read More
 NI RASMI SASA NADIA MUKAMI ANA UJA UZITO WA MPENZI WAKE ARROW BWOY

NI RASMI SASA NADIA MUKAMI ANA UJA UZITO WA MPENZI WAKE ARROW BWOY

Malkia wa muziki nchini Nadia Mukami pamoja na mpenzi wake Arrow Boy wanatarajiwa kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni. Wapenzi hao wawili wamethibitisha taarifa hiyo kwenye uzinduzi wa wakfu wao uitwao Lola na Safari ambao unalenga kuwasaidia akina mama wachanga kupata huduma nzuri ya afya ya uzazi. Lakini pia wamedokeza kuwa walipata wazo la kuja na wakfu wa Lola na Safari kipindi ambacho Nadia Mukami alipoteza uja uzito wake mwaka wa 2021, hivyo wana mpango wa kuzindua kituo cha kuwahudumia akina mama wachanga ambao ukutana na changamoto wakati wa uja uzito. Nadia Mukami amekuwa akikanusha madai ya kuwa na uja uzito licha ya mashabiki kusisitiza kuwa ana mimba ya Arrow Boy kutokana na kitendo chake cha kuvalia mavazi makubwa. Utakumbuka Mapema mwaka huu hitmaker huyo wa ngoma ya maombi alifunguka kuwa alipoteza uja uzito wake mwaka wa 2021 lakini akahamua kutoweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake. Mwezi agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu ambapo walienda mbali zaidi na kueleza kuwa waliahamua kuyaweka wazi mahusiano yao kwa sababu tayari walikuwa wamekuwa kiakili kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Read More
 NADIA MUKAMI ANYOSHA MAELEZO KUHUSU TETESI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKE ARROW BOY

NADIA MUKAMI ANYOSHA MAELEZO KUHUSU TETESI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKE ARROW BOY

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amekanusha madai ya kumu unfollow mchumba wake Arrow Boy kwenye mtandao wa Instagram. Akijibu shabiki yake kwenye mtandao wa instagram aliyetaka kujua hali ya uhusiano wake kwa sasa na Arrow Boy, Nadia Mukami amesema hajawahi fuatilia na Arrow Boy kwenye mtandao huo huku akithibitisha kuwa uhusiano wake na hitmaker huyo wa ngoma ya Unconditional Love upo imara licha ya uvumi unaosambaa mitandaoni kuwa hawana maelewano mazuri. Nadia Mukami ameyaweka hayo wazi wakati akitangaza ujio wa album mpya  ya Arrow boy iitwayo Focus inayotarajiwa kuingia sokoni machi 12 mwaka wa 2022. Mapema wiki hii mitandao nyingi ya udaku nchini iliripoti kuwa uhusiano wa Nadia Mukami na Arrow Boy umeingia na ukungu mara baada ya wasanii hao kutoonekana wakifuatilia kwenye mtandao wa Instagram. Utakumbuka Mwezi agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu. Hitmaker huyo wa Maombi alienda mbali na kueleza kuwa aliahamua kuyaweka wazi mahusiano yake na Arrow Boy kwa sababu tayari alikuwa amekuwa kiakili kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Read More
 NADIA MUKAMI AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI SEVENS HUB CREATIVE

NADIA MUKAMI AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI SEVENS HUB CREATIVE

Uongozi wa lebo ya Sevens Hub Creative umemtambulisha msanii wao mpya. Lebo hiyo inayomilikiwa na msanii Nadia Mukami imemtambulisha msanii aitwaye latinoh mwenye umri wa miaka 21 kutoka Likoni, Mombasa kuwa msanii mpya chini ya lebo hiyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia Mukami amemtambulisha msanii huyo kwa kuandika ujumbe wa kumsifia akisema kuwa uwezo wake wa kuandika nyimbo, melody na vocals ndio baadhi ya vitu vilivyomshawishi kumsajili latinoh kwenye lebo ya Sevens Bub Creative. Hitmaker huyo “Wangu” amewataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo kwenye tasnia ya muziki nchini lakini pia wakae mkao wa kula kupokea nyimbo zake. Tayari Latinoh  ameachia wimbo wake mpya uitao Siwezi ambao amemshirikisha Nadia Mukami na unapatikana kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni. Lebo ya Sevens Creative Hub ni kati ya lebo kubwa nchini Kenya ambazo zinafanya vizuri kwa sasa.

Read More
 NADIA MUKAMI KUMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA MWEZI FEBRUARI 2022

NADIA MUKAMI KUMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA MWEZI FEBRUARI 2022

Msanii nyota nchini Nadia Mukami ametangaza kumsaini msanii wake mpya chini lebo ya muziki ya Sevens Creative Hub mwezi Februari mwaka huu wa 2022. Kupitia ukurasa wake wa instagram amesema atamtambulisha msanii wake mpya chini ya Seven creative huo Februari mosi mwaka wa 2022 ambapo amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kumpokea msanii huyo ambaye pia ataachia video ya wimbo wake mpya ambayo amemshirikisha baada ya utambulisho wake. Verified Introducing our new artist 1st February 2022. In the first release, I feature the artist. New Music video loading…… @sevenscreative_hub For more details email: info@sevenscreativehub.com #AfricanPopStar #JengaSanaaNaSevens Hata hivyo wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda msanii huyo akawa Ssaru ambaye kipindi cha nyuma alinukuliwa kwenye instagram yake akisema mapema mwaka huu atasainiwa na lebo ya Sevens Creative hub ambayo inamilikiwa na Nadia Mukami.  

Read More