Msanii wa muziki wa Genge, Mejja, ametangaza kuwa albamu yake ya kwanza, ambayo awali ilikuwa imepangwa kutolewa mwaka huu, imeahirishwa hadi mwaka 2026.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mejja amefichua kuwa mradi huo umekuwa ukitengenezwa kwa zaidi ya miaka miwili, na amewahakikishia mashabiki kuwa utakuwa mkubwa zaidi katika taaluma yake ya muziki.
Msanii huyo, ameongeza kuwa albamu hiyo itabeba ladha halisi ya muziki wa Genge, ikiwa na ujumbe wa kipekee unaoakisi maisha halisi ya mashabiki wake.
Mejja amesema kuwa mashabiki wake tayari wamesikia baadhi ya vibao vilivyomo kwenye albamu hiyo na wamevutiwa navyo, akiahidi kuendelea kuwapa burudani kali wakati akisubiri kukamilisha mradi huo mkubwa.