Entertainment

Zuchu: Sipo Kwenye Mashindano ya Muziki

Zuchu: Sipo Kwenye Mashindano ya Muziki

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu, ameonyesha wazi kukerwa na kitendo cha mashabiki na wadau wa tasnia ya muziki wanaoendelea kumshindanisha na wasanii wengine mtandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Story, Zuchu amechapisha ujumbe wa kimafumbo uliodhihirisha msimamo wake kuhusu mashindano ya kisanii.

Katika ujumbe huo, amesisitiza kuwa yupo kwenye safari yake binafsi ya muziki na hana mpango wa kushindana na mtu yeyote, jambo lililoonyesha wazi kuchoshwa kwake na mijadala hiyo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Walimwengu kuanza kulinganisha wimbo wake mpya “Reason” na kazi za wasanii wengine wa Bongo Fleva, wakidai kuwa wimbo huo haujapata mapokezi makubwa kama ilivyokuwa kwa nyimbo zake za awali zilizovunja rekodi kwenye majukwaa ya kidijitali.

Ujumbe wa Zuchu umetafsiriwa na wengi kama msisitizo wa kauli yake ya mwaka wa 2022 ambapo alinukuliwa akisema kwamba hataki kabisa kushindanishwa na wasanii wa kike maana ngoma zake zipo kwenye ligi ya wasanii wa kiume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *