
Majina ya mastaa mbalimbali yametajwa kuwania tuzo za Mtv Europe Music mwaka wa 2021 ambazo zitafanyika nchini Hungury mwishoni mwa mwaka huu.
Kwenye orodha hiyo staa wa muziki kutoka Tanzania diamond platnumz ndiye msanii anayeiwakilisha Afrika Mashariki na kati.
Diamond Platnumz ametajwa kwenye kipengele cha Best African Act ambapo atachuana na wakali wengine kutoka Afrika kama wizkid, tems, focalistic na amaarae kutoka nchini Ghana.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa November 14,mwaka wa 2021 huko nchini Hungury. Justine Bieber ameongozwa kwa kutajwa kwenye vipengele vingi ambapo ametajwa kwenye vipengele nane.