Entertainment

Akeelah atangaza kuacha muziki

Akeelah atangaza kuacha muziki

Msanii wa kike kutoka Kenya Akeelah amezua gumzo mtandaoni baada ya kutangaza kuwa ameacha muziki kabisa.

Kupitia insta story yake Akeelah ameandika kuacha muziki kwa sababu ya maonevu na unyanyasaji alioupitia katika safari yake ya mziki.

Hitmaker huyo wa Tujikumbushe, ameushukuru uongozi wa Hakim Empire kwa mchango wao kwake huku akikosa kuutaja uongozi wa Shirko Media ambao ulimlea kimziki.

Akeelah hata hivyo ameondoa picha zake zote kwenye akaunti yake ya instagram, hii imeleta maswali na hisia kwa mashabiki zake kuwa inawezekana msanii huyo yupo mbioni kuachia kazi mpya za muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *