Entertainment

Buruklyn Wakanusha Kufanya Kazi na Toxic Lyrikali

Buruklyn Wakanusha Kufanya Kazi na Toxic Lyrikali

Mabingwa wa miondoko ya Drill kutoka Nairobi, Buruklyn Boyz, wameingilia kati na kuzima tetesi zilizoanza kusambaa kwa kasi mtandaoni zikidai kuwa kundi hilo linapika mradi mpya wa muziki na hasimu wao rapa Toxic Lyrikali.

Kupitia kurasa zao rasmi, Buruklyn Boyz wamekanusha vikali taarifa hizo na kudai kuwa hawana akaunti yoyote rasmi ya Facebook. Wamesema kuwa yeyote anayotumia jina lao kwenye jukwaa hilo ni tapeli anayepotosha mashabiki wao kwa taarifa za uongo.

Hata hivyo wasanii hao wametoa onyo kwa wafuasi wao kutokubali kudanganywa na akaunti feki (parody accounts) na kuwataka kufuatilia taarifa rasmi kupitia vyanzo vyao vilivyothibitishwa pekee.

Kauli hiyo imekuja kama pigo kwa mashabiki waliokuwa na shauku ya kuona kama bifu kati ya wasanii wa Buruklyn Boyz na rapa Toxic Lyrikali lingeweza kumalizwa kwa kazi ya pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *