Kundi la muziki la Buruklyn Boyz limeandika historia mpya baada ya albamu yao East Mpaka London kutunukiwa hadhi ya Gold Certification kufuatia kuvuka zaidi ya streams milioni 30 kwenye majukwaa mbalimbali ya kidijitali.
Kupitia ujumbe waliouchapisha mtandaoni, Buruklyn Boyz wamewashukuru mashabiki wao kwa mchango mkubwa walioonyesha tangu mwanzo wa safari yao ya muziki.
Albamu ya East Mpaka London iliachia rasm Mei 20 mwaka wa 2022 na ilikuwa albamu yao ya kwanza (debut album). Mradi huo ulijumuisha nyimbo 15, zikiwemo Pree, Dream Ya Kutoka Kwa Block, Catalyst, Usikam Hii Section, Blicky, Niskize na Coins.
Albamu hiyo pia iliwashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo Maya Amolo, Silverstone Barz, Big Yasa na Younglouie58, jambo lililoongeza utofauti wa sauti na ubunifu ndani ya mradi huo.
Mafanikio ya kupata Gold Certification yanaendelea kuthibitisha nafasi ya Buruklyn Boyz kama moja ya makundi yaliyochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa muziki wa drill nchini Kenya na Afrika Mashariki.