Staa wa muziki bongofleva Nandy amefunguka ya moyoni yale aliyoyapitia nchini Nigeria alipohudhurua halfa ya tuzo za Afrima mwaka wa 2021 zilizotolewa usiku wa Novemba 21.
Akiongea na Waandishi wa habari Nandy amesema, licha ya kukosa tuzo lakini yeye pamoja na mwimbaji mwenzake kutoka Tanzania, msanii Zuchu walionyeshewa dharau na kuchukuliwa poa wa kile alichokiita kutopata ‘treatment’ nzuri.
Nandy pia amefunguka namna Zuchu na wenzake walivyokosa sehemu yakupumzika siku waliyotua Nigeria kushuhudia hafla ya tuzo hizo.
Hata hivyo amesema kufuatia kupata mapokezi na uangalizi mbovu kutoka kwa waandaji wa tuzo za (AFRIMA) nchini Nigeria, anafikiria kuanzisha tuzo zake
Utakumbuka Nandy na Zuchu walikuwa wanawania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki katika tuzo za AFRIMA 2021 ambacho ushindi ulienda kwa Nikita Kering wa Kenya.