Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bennie Gunter amesainiwa chini ya lebo ya muziki ya Talent Africa group ambayo inasimamiwa na Aly Bhai.
Msanii huyo anaamini wasanii wanaweza afikia malengo yao bila ya kuwa na uongozi ikilinganishwa na mameja ambao hawawezi kukaa kwenye biashara ya muziki bila uwepo wa wasanii.
Gunter amesema wasanii wana uwezo mkubwa wa kufanikiwa kimuziki bila uwepo wa mameneja kama watajiamini na kuweka bidii kwenye kazi zao za muziki.
Hitmaker huyo wa “No letting Go” amesema majukumu pekee ya mameneja ni kutangaza na kusambaza nyimbo za wasanii ila wasanii wana nafasi kubwa ya kutanua wigo wa muziki wao.