Rapa kutoka Marekani Kanye West ana mpango wa kuipeleka Sunday Service nchini Urusi kwa mara ya kwanza.
Mtu wake wa karibu ameiambia tovuti ya Billboard kwamba YE amepanga kukutana na Rais Vladimir Putin kwa ajili ya mazungumzo.
Kwa mujibu wa Billboard Kanye West anataka kuweka makazi yake ya pili nchini Urusi pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ya kibiashara.
Ikumbukwe Sunday Service ni huduma ya kiroho ambayo huongozwa na rapa Kanye West ambapo hubadilisha nyimbo za kidunia kuwa nyimbo za kumsifu Mungu.