Sports news

Arsenal Yatinga Robo Fainali ya FA Cup kwa Ushindi Dhidi ya Mansfield Town

Arsenal Yatinga Robo Fainali ya FA Cup kwa Ushindi Dhidi ya Mansfield Town

Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la FA (FA Cup) baada ya kupata ushindi wa tabu wa mabao 2-1 dhidi ya Mansfield Town katika mchezo uliopigwa leo, Machi 7, 2026, kwenye uwanja wa One Call Stadium

Arsenal walitangulia kwa bao safi la Noni Madueke dakika 41 baada ya kazi nzuri ya pamoja, bao lililodumu hadi mapumziko. Mansfield Town walirejea kwa kasi kipindi cha pili ambapo mchezaji wa akiba, Will Evans, alileta mshangao uwanjani kwa kufunga bao la kusawazisha dakika 50 na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Baada ya hali kuwa ngumu, Arteta alimuingiza Eberechi Eze ambaye alihitaji dakika chache tu kupachika bao la ushindi dakika ya 66 na kuzima ndoto za Mansfield. Ushindi huo ni wa tano mfululizo kwa Arsenal katika mashindano yote, ukiendeleza kasi yao nzuri ya msimu huu ambapo pia wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu (EPL) kwa pointi 67.

The Gunners sasa wanageuza macho yao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League). Watasafiri kuvaana na Bayer Leverkusen nchini Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora, utakaopigwa Jumatano, Machi 11, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *