Entertainment

Eric Omondi Afunguka Kiasi Kikubwa cha Fedha Alichowahi Kupata Kupitia Wakfu wa Sisi kwa Sisi

Eric Omondi Afunguka Kiasi Kikubwa cha Fedha Alichowahi Kupata Kupitia Wakfu wa Sisi kwa Sisi

Mchekeshaji na mwanaharakati, Eric Omondi, amesema kiasi kikubwa zaidi kuwahi kukusanywa kupitia mpango wa Sisi Kwa Sisi ni shilingi milioni 15.7 za Kenya, zilizokusanywa ndani ya siku moja na nusu pekee.

Akizungumza kwenye podcast ya Chris The Bass, Omondi amesema fedha hizo zilikusanywa hivi karibuni kwa ajili ya kumsaidia mwanamke mmoja kutoka Githurai, ambaye kupitia mchango huo waliweza kumjengea nyumba za kupanga.

Omondi amesema aliweka namba ya malipo ya paybill mtandaoni wakati akiwa anasafiri kuelekea Kisumu kwenye moja ya hafla, na baada ya kutua kisumu ndani ya dakika 26, akaunti ya miamala ya simu ilikuwa tayari imepokea zaidi ya shilingi milioni 7.2

Mchekeshaji huyo, ameeleza kuwa mpango wa Sisi Kwa Sisi umeendelea kugusa maisha ya wengi, huku akibainisha kuwa michango mingi hutolewa na Wakenya kwa moyo wa kujitolea, ikiwa ni kiasi ndogo kama shilingi tano, kumi, ishirini au hamsini.

Kwa mujibu wa Eric Omondi, kutokana na maoni ya Wakenya, mpango huo sasa umejikita zaidi kusaidia matukio ya dharura, hasa kwa watu wasiokuwa na uwezo wa kujisaidia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *