Mwanamuziki nyota wa Uganda Jose Chameleone amekubali kuvunja rasmi ndoa yake ya miaka 17 na mkewe Daniella Atim, waliyoifunga Juni 7, mwaka 2008 na kubarikiwa watoto watano.
Daniella alifungua shauri la talaka Machi mwaka huu akidai kutelekezwa, kukosa upendo na msaada, hali iliyomsababisha msongo wa mawazo. Anataka umiliki wa nyumba ya Seguku, malezi ya watoto, msaada wa kifedha, pamoja na Chameleone kubeba gharama za mahakama.
Kwa upande wake, Chameleone anataka nyumba ibaki mali ya familia na aendelee kuwaona watoto. Pia amekanusha madai ya kutelekeza familia, akisema alishiriki kuhamisha familia Marekani mwaka 2018 na ameendelea kutoa msaada.
Kesi hiyo sasa inaendelea katika mahakama ya Kampala, huku ikiendelea kuvuta hisia kubwa nchini Uganda kutokana na hadhi ya wawili hao katika jamii na tasnia ya muziki.