Msanii nyota wa muziki nchini Uganda, Pallaso, amemshambulia vikali Bebe Cool, akimtuhumu kuwa mtu mwenye ubinafsi, chuki, na asiyethamini wasanii wenzake.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini humo, Pallaso amefichua kuwa licha ya kupatanishwa na Bebe Cool mwaka jana kupitia ushawishi wa Jose Chameleone, urafiki wao haukudumu kwa muda mrefu.
Ameeleza kuwa alikubali kutumbuiza bila malipo katika tamasha la Kiwatule Concert lililoandaliwa na Bebe Cool kama ishara ya upatanisho, lakini badala ya kuthamini juhudi hizo, Bebe Cool hakumshukuru wala kumpa chochote.
Pallaso amesema kuwa alisikitishwa zaidi baada ya kusikia Bebe Cool akimzungumzia vibaya kwenye vyombo vya habari, jambo alilolichukulia kama usaliti mkubwa kutoka kwa mtu aliyemwamini tena baada ya miaka minane ya kutokuelewana.
Msanii huyo wa wimbo “Malamu” ameongeza kuwa haoni tena uwezekano wa kuwa marafiki na Bebe Cool, akisisitiza kuwa sasa wamegeuka kuwa maadui wakubwa, sawa na uhasama wake na msanii Alien Skin.