Gossip

Muonekano wa Zuchu Wazua Tetesi za Ujauzito Mtandaoni

Muonekano wa Zuchu Wazua Tetesi za Ujauzito Mtandaoni

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Zuchu amezua gumzo mitandaoni baada ya kudaiwa kuwa ni mjamzito, kufuatia muonekano wake katika hafla ya Siku ya Wapendanao Duniani aliyohudhuria akiwa na mume wake, Diamond Platnumz.

Katika picha na video zilizosambaa mtandaoni, baadhi ya mashabiki wamedai kuona mabadiliko katika mwonekano wa msanii huyo, jambo lililochochea uvumi kuwa huenda wawili hao wanatarajia kupata mtoto. Wapo wanaodai mavazi aliyochagua pamoja na namna alivyokuwa akijishika tumbo vilichochea zaidi uvumi huo.

Wakati mjadala huo ukiendelea, wapo pia wanaodai kuwa kitendo cha Zuchu kuwajibu kwa ukali mashabiki wake na kuwazuia (ku-block) baadhi ya wanablogu wanaomkosoa huenda ni dalili ya jambo kubwa linaloendelea nyuma ya pazia.

Kwa sasa, suala la ujauzito linabaki kuwa tetesi zinazozungumzwa mtandaoni, huku wengi wakisubiri uthibitisho kutoka kwa Zuchu na mume wake Diamond Platnumz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *