Entertainment

Lady Jaydee Awashukuru Mashabiki kwa Kumheshimisha Baada ya Kujaza Ukumbi

Lady Jaydee Awashukuru Mashabiki kwa Kumheshimisha Baada ya Kujaza Ukumbi

Malkia wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jaydee, ameshindwa kujizuia na hisia za furaha baada ya mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kuhudhuria show yake maalum ya Valentine aliyoandaa pamoja na bendi yake jijini Dar es Salaam.

Katika usiku huo wa mahaba uliosheheni burudani ya moja kwa moja, Lady Jaydee alionekana kuguswa sana na namna ukumbi ulivyofurika mashabiki waliokuja kumuunga mkono.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Lady Jaydee amewashukuru mashabiki wake kwa kumheshimisha na kuonyesha kuwa bado wanaithamini kazi yake. Amesema kuwa mwitikio mkubwa alioupata ni uthibitisho kuwa bado ana nafasi kubwa mioyoni mwa wapenzi wa muziki, na kuwa muziki mzuri hauzeeki.

Katika ujumbe wake, msanii huyo hakusita pia kuwatumia ujumbe wale ambao wamekuwa wakimchukulia poa kwenye muziki, akisema kuwa nguvu ya mashabiki ndiyo inayompa motisha wa kuendelea kupambana na kutoa kazi bora zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *