Entertainment

Ringtone Amkosoa Guardian Angel kwa Kushindwa Kukemea Maovu Kwenye Jamii

Ringtone Amkosoa Guardian Angel kwa Kushindwa Kukemea Maovu Kwenye Jamii

Msanii wa injili Ringtone ametikisa mitandao ya kijamii baada ya kumkosoa vikali Guardian Angel, akidai ameshindwa kuwatumia vyema wasanii wa injili katika kupaza sauti dhidi ya maovu yanayoikumba jamii.

Ringtone anasema kwamba Guardian Angel, ambaye ni mmoja wa majina makubwa katika muziki wa injili nchini, ameshindwa kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa kiroho katika tasnia hiyo.

Kwa mujibu wa Ringtone, wasanii wa injili wanapaswa kuwa mstari wa mbele kukemea uovu, kuhamasisha maadili, na kuongoza jamii kuelekea mabadiliko chanya.

Msanii huyo anadai kuwa Guardian Angel ameiacha tasnia ikipoteza mwelekeo na matendo yake hayalingani na wajibu mkubwa alionao kwa mashabiki na jamii.

Ringtone anamtuhumu Guardian Angel kwa kuweka mkazo kwenye shughuli zisizoendana na wito wake wa muziki wa injili, akimtaja kuwa “failure” anayefanya kazi ambazo tayari zina wataalamu wake.

Haya yanajiri wakati mjadala kuhusu nafasi ya wasanii wa injili katika kupaza sauti dhidi ya maovu ukiendelea kushika kasi, huku mashabiki wakigawanyika kuhusu nafasi halisi ya wasanii katika masuala ya kijamii na kiroho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *