Entertainment

Museveni Amshauri Alien Skin Aachane na Muziki Kama Umemshinda

Museveni Amshauri Alien Skin Aachane na Muziki Kama Umemshinda

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amempa onyo kali msanii mwenye utata Alien Skin baada ya msanii huyo kuonekana hadharani akipinga baadhi ya sera za serikali kupitia muziki na majukwaa yake ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na msanii huyo kwenye ikulu jijini Kampala, amemshauri msanii huyo kama anaona muziki unamlemea au hauendani na dhamira ya kujenga jamii, basi ni busara kwake kuachana nao mapema.

Rais huyo amemuelekeza Alien Skin kujikita katika shughuli nyingine za kujitegemea kama kilimo, akisema sekta hiyo ina mchango mkubwa katika uchumi wa taifa na haina migongano kama ile inayojitokeza kwenye muziki wenye ujumbe tata.

Rais Museveni ameonya kuwa kutumia sanaa kama jukwaa la kupinga juhudi za maendeleo ni sawa na kuwa kikwazo kwa mustakabali wa taifa. Amewataka wasanii kutumia vipaji vyao kuhimiza umoja, uzalendo na maendeleo ya taifa badala ya kueneza ujumbe unaoweza kuwagawanya vijana au kuchochea chuki dhidi ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *