Eddy Kenzo Amtaka Bebe Cool Kuachia Nyimbo Badala ya Kugeukia Content Creation
Msanii nyota wa Uganda Eddy Kenzo amemtaka mkongwe wa muziki nchini humo Bebe Cool kurejea studio na kuachia ngoma kali, badala ya kujikita zaidi katika utengenezaji wa maudhui (content creation) mitandaoni. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Eddy Kenzo amesema ni jambo la kusikitisha kuona msanii mwenye historia kubwa kama Bebe Cool akigeukia zaidi kazi za kutengeneza content na kuwakosoa wasanii wengine, badala ya kutumia uzoefu na kipaji chake kuendelea kuutumikia muziki kwa kutoa vibao vipya. Kenzo ameongeza kuwa Bebe Cool ana mchango mkubwa katika muziki wa Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla, hivyo mashabiki bado wana matarajio makubwa ya kusikia kazi mpya zenye ubora kutoka kwake. Aidha, Eddy Kenzo amemtaka Bebe Cool kuwaachia vijana wa Gen Z jukumu la kutengeneza content mitandaoni, akisisitiza kuwa kizazi hicho ndicho chenye nguvu na ubunifu mkubwa katika eneo hilo, huku wasanii wakongwe wakipaswa kubaki kwenye msingi wao wa muziki.
Read More