Entertainment

Eddy Kenzo Aahidi Mabadiliko Makubwa Kwa Wasanii Uganda

Eddy Kenzo Aahidi Mabadiliko Makubwa Kwa Wasanii Uganda

Staa wa muziki kutoka Uganda, Eddy Kenzo, ameibua matumaini mapya kwa wasanii baada ya kutangaza kuwa serikali imeipa kipaumbele marekebisho ya sheria ya hakimiliki ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

Kenzo ambaye ni rais wa shirikisho la wasanii nchini Uganda, amesema kuwa muswada huo utashughulikiwa mara tu Bunge la mwaka 2026 litakapoketi rasmi kuanza kazi.

Kwa mujibu wa Kenzo, mfumo mpya wa usimamizi wa hakimiliki tayari umeidhinishwa, na kilichosalia sasa ni kutoa elimu kwa wadau ili utekelezwe kikamilifu. Amebainisha kuwa serikali, ikiwemo Rais Yoweri Museveni, imeamua kulipa suala hilo uzito wa juu kwa manufaa ya tasnia nzima ya muziki.

Hata hivyo amewataka wasanii na wadau wa burudani kuendelea kumuunga mkono Rais Museveni katika uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa mabadiliko yanayotarajiwa kwenye sheria mpya za hakimiliki yatawaletea fursa bora za kifedha na kulinda kazi zao dhidi ya wizi wa kimtandao.

Hatua hii imeonekana kama mwanga wa matumaini kwa wanamuziki na watayarishaji wa muziki nchini Uganda, ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakipigania mfumo madhubuti wa kulinda haki zao za kiubunifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *