Jose Chameleone na Juliet Zawedde Wazua Gumzo kwa Mabusu Jukwaani

Jose Chameleone na Juliet Zawedde Wazua Gumzo kwa Mabusu Jukwaani

Staa wa muziki kutoka Uganda, Jose Chameleone, amezua mjadala mpya mtandaoni baada ya kuonekana akiwa na ukaribu wa kimahaba na mfanyabiashara maarufu anayeishi Marekani, Juliet Zawedde, katika tamasha la usiku lililofanyika jana. Wawili hao, ambao uhusiano wao wa karibu umekuwa ukileta minong’ono kwa muda mrefu, waliibua shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki waliokuwa ukumbini baada ya kubusiana hadharani jukwaani, hali iliyowafanya mashabiki kuzidi kudai kwa sauti kuwa uhusiano wao upewe hadhi rasmi ya ndoa. Zawedde aliwasili Uganda wiki iliyopita kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, huku sherehe kuu ikifanyika Julai 19 katika klabu ya Noni Vie jijini Kampala. Hata hivyo, Chameleone hakuweza kuhudhuria tukio hilo kutokana na kuwa safarini mjini Bujumbura. Lakini jana usiku, wawili hao walipata nafasi ya kukutana tena jukwaani, na tukio hilo lilibadilika kuwa burudani ya kipekee kwa mashabiki waliokuwa wamehudhuria. Video inayosambaa kwa kasi mitandaoni inaonesha Zawedde akipanda jukwaani, kumkumbatia Chameleone kwa nguvu, kisha kumbusu kwa mikono miwili usoni mbele ya umati mkubwa uliokuwa ukishangilia. Kitendo hicho kimewasha moto mpya kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mashabiki wengi wamekuwa wakiandika maoni ya kuwataka wawili hao kuhalalisha penzi lao. Hadi sasa, hakuna mmoja kati yao aliyetoa kauli rasmi kuhusu hatua inayofuata katika uhusiano wao, lakini wazi ni kwamba mashabiki wao wana matumaini makubwa kuona penzi hili likibadilika kutoka ‘urafiki wa karibu’ na kuwa rasmi zaidi. Hii si mara ya kwanza wawili hao kuhusishwa kimapenzi, lakini tukio la jana linaonekana kama uthibitisho mpya wa ukaribu wao unaozidi kushika kasi mbele ya macho ya umma.

Read More
 Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametangaza nia yake ya dhati ya kushirikiana na msanii mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone, katika wimbo mpya unaotarajiwa kutoka mwaka huu. Akiwa jukwaani katika tamasha la Coffee Marathon huko Ntungamo, Uganda, Diamond aliwajulisha mashabiki kuwa kolabo hiyo ni ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu, na sasa anafanya kila juhudi kuhakikisha inatimia. Diamond alisema kuwa licha ya mafanikio yake makubwa katika bara la Afrika, hajawahi kusahau mchango wa Jose Chameleone katika muziki wa Afrika Mashariki. Alimuelezea kama msanii aliyeathiri kizazi kizima na kumvutia hata yeye kuingia kwenye tasnia ya muziki. “Mwaka huu nataka kuhakikisha ninafanya wimbo na Jose Chameleone. Tunamshukuru Mungu kuwa anaendelea vizuri kiafya na tunamshukuru kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki,” alisema Diamond mbele ya mashabiki. Kwa upande wake, Jose Chameleone, ambaye ametamba kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki kuwa moja ya nguzo za muziki wa Afrika Mashariki, bado anaheshimika kwa nyimbo zake zenye ujumbe mzito na sauti ya kipekee. Kolabo kati ya Chameleone na Diamond inatarajiwa kuwa ya kihistoria, na tayari mashabiki kote kanda ya Afrika Mashariki wanasubiri kwa hamu kusikia kazi yao ya pamoja.

Read More
 Chameleone adokeza mpango wa kubuni bendi ya muziki ya familia

Chameleone adokeza mpango wa kubuni bendi ya muziki ya familia

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amefichua mpango wa kuunda bendi ya familia itakayojumuisha ndugu zake, Pallaso na Weasel. Katika mahojiano hivi karibuni, Chameleone ameeleza kuwa watatu hao bado wapo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kufikia makubaliano. Bendi hiyo huenda ikazinduliwa hivi karibuni katika hafla itakayofanyika jijini Kampala, katika uwanja wa Namboole. “Tunapanga kuanzisha bendi ya familia na tutatoa mweelekeo hivi karibuni. Uzinduzi huo unahitaji ukumbi mkubwa ambao hauko tayari kwa sasa. Tunataka eneo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya watu 40, 000,” alisema. Jose Chameleone ameweka wazi hayo kwenye mkao na waandishi wa habari wakati akielezea mipango yake juu  tamasha lake “Gwanga Mujje” litakalofanyika huko Lugogo Cricket Oval mwezi Februari mwaka huu.

Read More
 Uongozi wa Jose Chameleone wafunguka kuhusu tuhuma za msanii huyo kumpiga Boda Boda

Uongozi wa Jose Chameleone wafunguka kuhusu tuhuma za msanii huyo kumpiga Boda Boda

Menejimenti ya Mwanamuziki Jose Chameleone kupitia Afisa Uhusiano wake, imetoa maelezo kuhusiana na video ambayo imetoka ikimuonesha mwimbaji huyo maarufu wa nchini Uganda akimpiga mhudumu wa boda boda. Taarifa hiyo imeeleza kwamba tukio hilo lilitokea November 12, mwaka 2022 ambapo mwendesha boda boda huyo aliichuna kwa pembeni gari ya Jose Chameleone aina ya Range Rover. Taarifa hiyo iliendelea kusema, Chameleone angeweza kupuuzia tukio hilo kama sio maneno ya matusi na vitisho kutoka boda boda huyo. Tukio linaloonekana ni Jose Chameleone akijaribu kujilinda mwenyewe dhidi ya mwendesha boda boda huyo ambaye alikuwa akimfuata kwa shari. Aidha taarifa ya menejimenti ya Chameleone inakamilika kwa kulaani kitendo hicho.

Read More
 Rapa Gravitty Omutujju afufua bifu yake na Jose Chameleone

Rapa Gravitty Omutujju afufua bifu yake na Jose Chameleone

Rapa kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amefufua tena bifu yake na msanii mkongwe Jose Chameleone. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Omutujju amesema hana mpango kumuunga mkono Chameleone kwenye shoo yake ijayo, itakayofanyika huko Lugogo, Cricket Oval. Gravity Omutujju amesema shoo ya msanii huyo itabuma vibaya huku akidai kwamba hatokuja kumheshimu Jose Chameleone kwa sababu hajawahi kumfanyia kitu chochote kizuri kwenye maisha yake. “Siwezi kumuunga mkono, hajawahi kunisaidia kwa namna yoyote ile. Mwache apambane na hali yake, asitarajie msaada kutoka kwangu. Sijali hata kuhusu onesho la Chameleone kwa sababu si mtu mzuri,” alisema.

Read More
 King Saha amshukuru Chameleone kwa kusimama naye wakati wa matatizo

King Saha amshukuru Chameleone kwa kusimama naye wakati wa matatizo

Mwanamuziki King Saha ni mwingi wa shukran kwa kitendo cha Jose Chameleone kutumbuiza kwenye shows zake alizokuwa ameratibu kutoa burudani kwa mashabiki zake. King saha ambaye aliruhusiwa kuondoka katika hospitali ya Nakasero wiki iliyopita ambako alikuwa amelazwa, amefarijika na ukarimu waBosi huyo wa Leone Island kumkingia kifua alipokuwa kwenye matatizo ambapo amemtaja kuwa mtu mwema kuwahi kutokea nchini Uganda kwa upande wa wasanii. “Namshukuru Chameleone kwa ukarimu wake. Namheshimu sana kwa kunifanyia shows zangu nilipokuwa nimelazwa hospitalini,” alisema. King Saha kwa sasa amechukua mapumziko kwenye muziki wake kwa ajili ya kuiweka afya yake sawa kabla ya kuanza shughuli zake rasmi.

Read More
 Niko tayari kutumbuiza katika shoo zote za King Saha hadi atakapopata nafuu- Chameleone

Niko tayari kutumbuiza katika shoo zote za King Saha hadi atakapopata nafuu- Chameleone

Msanii mashuhuri kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amejitolea kujaza nafasi ya mwanamuziki King Saha katika shoo zake zote alizokuwa ameratibiwa kutumbuiza  hadi atakapopata afueni. Katika mahojiano hivi karibuni, Chameleone amesema yuko tayari kuwapa burudani mashabiki wake bure bila malipo. Bosi huyo wa Leone Island ameeleza kuwa tayari ameanza mazungumzo na meneja wa King Saha aitwaye Mukasa ili kufanikisha hilo. “Sasa hivi mdogo wangu King Saha hayuko vizuri kiafya na tayari nimempigia simu meneja wake, Mukasa kuhusu pendekezo langu. Nitatumbuiza kwenye shoo zake vya alizopewa nafasi bila bila malipo. Huu ni wakati ambao anahitaji wema wetu,” alisema Chameleone. King Saha aliruhusiwa kwenda nyumbani siku ya Jumanne kutoka hospitali ya Nakasero ambapo alishauriwa na madaktari kupumzika kabla ya kuanza tena shughuli zake za muziki.

Read More
 Jose Chameleone atakiwa kuzindua kampuni yake ya simu

Jose Chameleone atakiwa kuzindua kampuni yake ya simu

Msanii mkongwe kutoka nchini Uganda Jose Chameleone ameshauriwa kutekeleza mpango wake wa kuanzisha mradi wake kufungua kampuni ya simu iitwayo Chameleone Phones. Wito huo umetolewa na mwanahabari Douglas Lwaga ambaye amehoji kuwa Chameleone alipoteza fursa kubwa ya kuingiza pesa nyingi kupitia mpango wake wa kuzindua kampuni ya simu. Hata hivyo amesema msanii huyo mkongwe ana nafasi nyingine ya kufaulu kibiashara kupitia wazo lake hilo kwa kuwa ana bado ana ushawishi kwenye tasnia ya muziki Afrika mashariki na barani Afrika kwa ujumla. “Jose Chameleone missed out on a huge opportunity of launching the Chameleone Phone. This could have brought him lots of cash. I think he can still go for it,” Alisema kwenye kipindi cha runinga cha After 5 show. Utakumbuka zaidi mwongo mmoja uliopita Jose Chameleone alikuwa na mpango wa kuzindua kampuni yake ya simu iitwayo Chameleone Phone lakini hakufanikiwa kutekeleza mpango wake huo kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake.

Read More
 CHAMELEONE AANIKA SIRI ZA BOBI WINE

CHAMELEONE AANIKA SIRI ZA BOBI WINE

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha ya msanii aligeukia siasa Bobi Wine. Kwenye moja ya performance yake juzi kati, Chameleone amedai kwamba Bobi Wine hawezi tena toka nje ya ndoa yake kwa sababu anaogopa kuwekewa sumu. Hitmaker huyo wa Bolingo ya Nzambe amesema Bobi Wine anahofia sana wanawake kwa kuwa wanaweza tumiwa na watesi wake kumuangamiza. “Bobi Wine alikuwa jambazi kama mimi lakini sasa hawezi tena kufurahia maisha ya usiku jijini Kampala. Hata aliomba usalama kutoka kwa vyombo vya usalama kuhudhuria tamasha la Fik Fameika. Anaogopa kufanya mapenzi na wanawake wengine kwa sababu anaweza kulishwa sumu,” alisema. . Mwimbaji huyo ameongeza kuwa Bobi Wine anakosa maisha yake ya muziki ambayo yalikuwa yanampa huru wa kutangamana na mashabiki bila uoga wowote.

Read More
 CHAMELEONE AFUNGUKA KUHUSU BIFU YAKE NA BOBI WINE

CHAMELEONE AFUNGUKA KUHUSU BIFU YAKE NA BOBI WINE

Msanii mkongwe nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka uhusiano wake na Bobi Wine ambaye wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Chameleone amesema kwa sasa hana ugomvi wowote na msanii huyo aliyegeukia siasa kwa kuwa alishamsamehe zamani kwa hatua ya kunyima tiketi ya chama chake cha nup wakati alikuwa anawania wadhfa wa umeya wa jiji la kampala. “I have no problem with Bobi Wine and I cleansed my heart for whatever he did. I didn’t get the party ticket but I don’t mind about that anymore.” Amesema. Hitmaker huyo wa Forever ameeleza kuwa hawezi kubali  siasa iharibu uhusiano wake na Bobi Wine ambao wameujenga kwa kipindi kirefu ikizingatiwa kuwa wamekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 20. “I have known Bobi Wine for twenty years and our relationship matters most,” he said in an interview with local television.” Ameongeza Utakumbuka Chameleone na Bobi Wine mara ya mwisho kukutana ilikuwa kwenye birthday party ya mwanamuziki mwenzao Eddy Yaawe ambayo ilifanyika mwezi meo mwaka huu viungani mwa jiji la Kampala.

Read More
 CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOWANIA URAIS UMA

CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOWANIA URAIS UMA

Msanii mkongwe nchini Uganda Jose Chameleone amevunja ukimya wake kuhusu kutowania urais katika chama cha wanamuziki nchini humo UMA. Katika mahojiano yake hivi karibuni Chameleone amesema ameshikika sana kwenye kazi zake za muziki hivyo atapata nafasi ya kutekeleza majukumu ya chama cha wanamuziki nchini Uganda. Hitmaker huyo wa ngoma ya Forever amedai kuwa wasanii wanahitaji mtu ambaye ameshikika kikazi lakini pia ana muda wa kujishughulisha na majukumu ya chama hicho. “I would have contested to be UMA President but honestly am very busy for that. We need to find artists that are busy but can run the post as well”, –Jose Chameleone. Hata hivyo hajabainika ni lini hasa uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda utafanyika baada ya Wizara ya Leba, jinsia na masuala kijamii kuahirisha uchaguzi huo bila kutoa maelezo.

Read More
 CHAMELEONE NA BOBI WINE WAMALIZA TOFAUTI ZAO

CHAMELEONE NA BOBI WINE WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Mastaa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone na Bobi wine hatimaye wamemaliza ugomvi wao uliodumu kwa kipindi cha miaka miwili. Hii ni baada ya wawili hao kukutana kwenye hafla ya kusherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanamuziki eddy yawe mapema wiki ambapo walipata wasaa mzuri wakuzungumza huku wakionekana wakiwa na nyuso za tabasamu. Taarifa za Bobi wine na Chameleone kumaliza bifu yao imethibitishwa na Eddy Yawe  ambaye ni kaka wa Bob Wine kwa kusema kwamba amefurahishwa na hatua ya wawili wao kuitikia mwaliko wake huku akisisitiza waendelee kuwa marafiki licha ya utofauti wao wa kisiasa. Hata hivyo mashabiki wa muziki nchini Uganda wamewapongeza wawili hao kwa hatua ya kumaliza tofauti zao huku  wakiwataka waachie wimbo wa pamoja utakaothibitisha kuwa wamemaliza ugomvi wao. Utakumbuka  Chameleone aliingia kwenye ugomvi na Bobi Wine mwaka wa 2020 baada ya Bobi Wine kumnyima tiketi ya kuwania kiti cha umeya wa jiji la kampala  kupitia chama cha kisiasa cha NUP. Tangu wakati huo Chameleone amekuwa akimshambulia Bobi Wine pamoja na watu wake wa karibu kwa hatua ya kuwa kizingiti kwenye azma yake ya kuwa mwanasiasa.

Read More