Msanii mkongwe wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone, ametoa onyo kali kwa promota maarufu Nobart Events kufuatia matamshi yake ya mara kwa mara dhidi ya wasanii wa familia ya Mayanja.
Chameleone ameeleza kuwa hajawahi kufanya kazi na Nobart kama promota, na hivyo haoni sababu ya kushambuliwa hadharani. Ameonyesha kutoridhishwa na kile alichokitaja kama chuki na taarifa za uongo inayoenezwa dhidi yake, akisisitiza kuwa hatavumilia tena udhalilishaji huo.
Msanii huyo amesisitiza kuwa hana tatizo binafsi na Nobart lakini hatasita kumkabili endapo ataendelea kumhusisha kwa maneno ya kudhalilisha.
Onyo hilo limekuja baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya maneno kati ya Nobart na wana familia ya Mayanja, wakiwemo wasanii Pallaso na Weasel, ambao wote ni ndugu wa Chameleone.