Entertainment

Toxic Lyrikali Apuuza Diss track ya Pili ya Buruklyn Boyz kwa Kuita Mchongoano

Toxic Lyrikali Apuuza Diss track ya Pili ya Buruklyn Boyz kwa Kuita Mchongoano

Rapa kutoka Kenya Toxic Lyrikali ameendelea kushikilia msimamo wake wa kupuuza mashambulizi ya kimuziki kutoka kwa kundi la Buruklyn Boyz, akiwataka wasanii hao kuja na hoja mpya zenye ubunifu badala ya kurudia mashairi na mada zilizokwisha tumika.

Kupitia ujumbe aliouandika mitandaoni, Toxic ameonyesha kutoridhishwa na kiwango cha ubunifu kilichoonyeshwa kwenye diss track ya Buruklyn iitwayo Genje Sana, akidai kuwa maudhui yaliyomo kwenye diss hiyo ni ya zamani na haoni kitu kipya kinachoweza kumsukuma kujibu kile alichokiita mchongoano.

Msanii huyo amesemakuwa hataki kuhusishwa na masuala yasiyokuwa na tija, akieleza kuwa kwa sasa hana muda wa kujibu kile alichokiita diss track ya kijinga. Kwa mujibu wake, anajikita zaidi katika kukuza brand yake na kufanya muziki wenye malengo makubwa kuliko kuingia kwenye mijadala isiyo na manufaa.

Katika diss track ya Buruklyn Boyz iitwayo Genje Sana, wamekosoa vikali diss track ya Toxic iitwayo Dumpsite, wakidai kuwa wimbo huo ni duni na haukufikia viwango vya mashairi vinavyotarajiwa kwenye hip hop. Kundi hilo limemtaka Toxic atulie ili wamfunze namna ya kuandika mashairi makali, wakisisitiza kuwa wao wamemtangulia kwenye muziki na wana uzoefu mkubwa zaidi kwenye game.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *