Gossip

Akothee Alalamikia Kutozwa Gharama Kubwa za Urembo wa Kucha

Akothee Alalamikia Kutozwa Gharama Kubwa za Urembo wa Kucha

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, amelalamikia kutozwa gharama kubwa aliyodai hakuwa amepangia kwenye bajjeti yake baada ya kupata huduma ya urembo wa kucha.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Akothee amesema alishangazwa kutozwa pesa za huduma ya kupanga na kupaka rangi kucha pamoja na kulipishwa nauli ya teksi ya mtaalam wa urembo ilhali alikuwa amepangia kulipa gharama za huduma ya kucha pekee.

Kwa mujibu wake, gharama hiyo ilikuwa kubwa kupita kiasi ikilinganishwa na huduma aliyopokea, jambo lililomfanya aibue suala hilo hadharani.

Mwanamama huyo ameeleza kuwa hana pesa ya kugawa ovyo ovyo, akisisitiza kuwa fedha anazopata huzitumia kusaidia watu wenye uhitaji na miradi ya kijamii. Ameongeza kuwa ni muhimu kwa watoa huduma kuwa wazi mapema kuhusu gharama zote ili kuepuka sintofahamu kwa wateja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *