Gossip

Akothee Awakosoa Mastaa Wanaoishi Maisha ya Kuigiza Mtandaoni

Akothee Awakosoa Mastaa Wanaoishi Maisha ya Kuigiza Mtandaoni

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, amewakosoa vikali baadhi ya mastaa nchini humo kwa kile alichokiita kuishi maisha ya uongo kwenye mitandao ya kijamii.

Akothee anadai kuwa mastaa wengi wanajionyesha kama watu wenye utajiri mkubwa mtandaoni, lakini ukweli ni kwamba wengi wao hawana uwezo huo katika maisha ya kawaida.

Mwanamama huyo, amewataka mashabiki kutopoteza muda kujilinganisha na maisha ya watu wanaowaona mtandaoni, akisema maisha ya mtandaoni mara nyingi hayalingani na uhalisia.

Sanjari na hilo, Akothee amewakosoa baadhi ya content creators wanaotafuta umaarufu kwa kutumia matusi na kuwashambulia mastaa, akisema aina hiyo ya maudhui inachochea chuki na inakosa ubunifu. Amewahimiza kutengeneza maudhui yanayozingatia kazi yenye thamani badala ya kutegemea kiki za muda mfupi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *