Gossip

Thee Pluto Alalamikia Kunyimwa Kumwona Binti Yake Zoey

Thee Pluto Alalamikia Kunyimwa Kumwona Binti Yake Zoey

Mwanamitandao maarufu nchini Kenya, Thee Pluto, ameshindwa kujizuia na kuibua hisia kali mitandaoni baada ya kudai kwamba amekuwa akinyimwa fursa ya kumwona binti yake, Zoey.

Kwenye mahojiano na Obinna TV, Pluto amesema hali hiyo imekuwa ikimuumiza kwa muda mrefu huku akimtaja mama mzazi wa Felicity, ambaye ni mama mkwe wake, kama chanzo kikuu cha mgogoro huo wa kifamilia.

Thee Pluto ameeleza kwamba licha ya juhudi zake za kutaka kushiriki katika malezi ya binti yake, amekumbana na vikwazo vinavyomfanya ajihisi kutengwa. Kwa mujibu wake, amekuwa hakubaliwi kushiriki kikamilifu katika maisha ya Zoey, jambo analosema linamvunja moyo kama mzazi.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hana tatizo na Felicity moja kwa moja, bali anaamini kwamba ni mama mkwe anayekwamisha mawasiliano na mipango ya kumhudumia binti yao. Pluto amesema anatumai mgogoro huo utaweza kutatuliwa ili wampe Zoey mazingira bora ya malezi bila migongano ya kifamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *