Gossip

Baba Levo Akerwa na Tukio la Mfanyakazi wa Ndani Kumfanyia Ukatili Mtoto Wake

Baba Levo Akerwa na Tukio la Mfanyakazi wa Ndani Kumfanyia Ukatili Mtoto Wake

Msanii wa Bongo Fleva Baba Levo ameonyesha maumivu makubwa na kukerwa sana baada ya kanda ya CCTV kufichua tukio la ukatili lililofanywa na mfanyakazi wa ndani dhidi ya mtoto wake, Platnum, wakati yeye na mke wake hawakuwepo nyumbani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Baba Levo ameeleza jinsi tukio hilo lilivyomuathiri yeye na mke wake Mama Ruby, akisema kuwa video ya tukio hilo imeumiza sana familia yake.

Msanii huyo aliyegeukia siasa, amefunguka kwamba mara nyingi huwa anamwomba mke wake abaki nyumbani na watoto ili yeye aweze kushughulika na kazi zake, lakini mara nyingi ombi hilo huonekana kama jaribio la kumfanya mke wake kuwa tegemezi.

Hata hivyo, amesema video hiyo imempa mke wake maumivu makubwa na kuthibitisha umuhimu wa wazazi kuwa karibu na watoto wao.

Kauli ya Baba Levo inakuja mara baada ya kanda ya CCTV kumuonyesha mfanyakazi wake wa ndani akimfunga miguu mtoto wake, kitendo ambacho kimezua hasira na masikitiko makubwa kwa familia ya msanii huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *