Staa wa muziki kutoka Kenya, Bahati, amewaomba mashabiki wake pamoja na Wakenya kwa jumla kumpa mapumziko baada ya jina lake kuwa gumzo mitandaoni tangu arejee rasmi kwenye muziki wiki chache zilizopita.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Stories, Bahati ameonekana kuchoshwa na hali ya kutajwa kila mara mtandaoni, akisema kuwa tangu afanye kurejea kwake kwenye muziki amekuwa akitrend sana, na sasa anahisi imetosha. Amewaomba mashabiki wachukue msanii mwingine angalau naye apate nafasi ya kujadiliwa mitandaoni.
Kauli yake imekuja siku moja baada ya kushindwa kutimiza ahadi ya kufuta wimbo wake wenye utata uitwao Seti licha ya Wakenya kutimiza masharti aliyokuwa amewapa.
Bahati alikuwa ameahidi kwamba angefuta wimbo wake mpya Seti endapo angepata maoni (comments) zaidi ya 500 kwenye moja ya machapisho yake ya Instagram. Mashabiki walitimiza ahadi hiyo kwa muda mfupi, lakini msanii huyo hakufuta wimbo huo kama alivyoahidi.