Msanii wa muziki asiyeishiwa na matukio kila kuchao, Bahati, amezima tetesi zilizosambaa mtandaoni kuhusu baby mama wake, Yvette Obura, kuvishwa pete ya uchumba kupitia wimbo wake mpya uitwo First Love.
Katika video ya wimbo huo, Yvette Obura na mwanaume anayedaiwa kuwa mchumba wake wameonekana kama video queen na video king, wakicheza nafasi za wapenzi wawili waliokuwa katika mahusiano ya kimapenzi yenye hisia kali.
Hatua hiyo imewachanganya mashabiki wengi mtandaoni waliodhani kuwa Yvette amepata mchumba mpya, huku wengine wakihusisha tukio hilo na mbinu ya kuvutia hisia za mashabiki na kuongeza hamasa ya kutazamwa kwa video ya wimbo mpya wa Bahati, First Love.
Kwa sasa, video ya wimbo huo imezidi kupata umaarufu mkubwa mtandaoni hasa Youtube ambapo ina zaidi ya watazamaji laki tatu ndani ya siku moja.Wachambuzi wa masuala ya burudani wamemsifu Bahati kwa ubunifu wa kipekee katika kutumia stori ya maisha halisi kuchochea mjadala wa muziki wake.