Entertainment

Harmonize Atangaza Kuachia Kolabo Tatu Disemba 25, Ikiwemo Ngoma na Mbosso

Harmonize Atangaza Kuachia Kolabo Tatu Disemba 25, Ikiwemo Ngoma na Mbosso

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize, ametangaza rasmi kuwa ataachia ngoma tatu za kolabo tarehe Disemba 25 mwaka 2025, zikiwemo kazi zinazowahusisha wasanii wakubwa ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Kupitia Instagram stories, Harmonize amefichua kuwa miongoni mwa kolabo hizo ni ushirikiano wake wa kwanza kabisa na Mbosso. Katika maelezo yao kupitia mitandao ya kijamii, Harmonize na Mbosso wamezungumzia kwa pamoja mradi wao ujao, kila mmoja akimuelezea mwenzake kwa namna anavyomfahamu.

Harmonize amemtaja Mbosso kama msanii mwenye kipaji cha kipekee na sauti yenye hisia, huku Mbosso akimpongeza Harmonize kwa ubunifu, uthubutu na mchango wake mkubwa katika kupeleka muziki wa Bongo Fleva kimataifa.

Katika hatua nyingine, Harmonize pia ametangaza kuachia Kolabo na Focalistic, staa mkubwa kutoka Afrika Kusini pamoja na
Kolabo ya Yana Toma, ambayo pia inatajwa kuwa na ladha mpya na tofauti.

Kwa sasa, macho na masikio ya wadau wa muziki yameelekezwa Disemba 25, siku ambayo Harmonize anatarajiwa kuwapa mashabiki wake zawadi ya Sikukuu kupitia kolabo hizi tatu zinazosubiriwa kwa hamu kubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *