Kundi la Buruklyn Boyz, limeendelea kutikisa chati za muziki nchini Kenya kufuatia bifu lao na rapa Toxic Lyrikali ambalo linazidi kupamba moto mtandaoni.
Diss tracks zao zilizotolewa hivi karibuni zimeonyesha mafanikio makubwa kwenye majukwaa mbalimbali ya kidijitali ambapo wimbo wao “Genje Sana” umefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya Apple Music Top 100 Kenya, jambo linalodhihirisha jinsi mashabiki walivyoupokea kwa kasi.
Kwenye mtandao wa Youtube, wimbo wao mwingine wa kujibu mashambulizi, “Stima,” nao umeshika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya trending nchini Kenya, ukiwa tayari umetazamwa zaidi ya mara laki sita. Diss track hiyo imemshusha Toxic Lyrikali ambaye amekuwa akitawala chati za Youtube kwa muda hadi nafasi ya pili kupitia Diss track yake iitwayo Dumpsite ambayo ina views zaidi ya laki nne.
Wakati huo huo, Diss track ya Buruklyn Boyz iitwayo “Genje Sana” inashikilia nafasi ya nne kwenye chati hiyo ya YouTube Trending ikiwa na zaidi ya watazamaji laki tatu.