Msanii wa dancehall nchini Kenya, KRG The Don, amemshambulia vikali mrembo na mtangazaji Kendi baada ya kumkosoa kufuatia ushindi wake wa tuzo ya Dancehall Artist of the Year.
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, KRG amemtolea uvivu Kendi, akisema hana uelewa wowote kuhusu muziki wa dancehall na hana mamlaka ya kuzungumzia tasnia ya muziki.
Msanii huyo amesema kuwa ushindi wake ni halali na umetokana na juhudi, kazi ngumu pamoja na mchango wake mkubwa katika kukuza dancehall nchini Kenya.
Mbali na hilo, KRG amemshauri Kendi ajikite katika majukumu ya kumhudumia mume wake badala ya kuingilia masuala ya muziki, akidai muda wake kwenye tasnia tayari umepita.
Kauli ya Kendi imekuja mara baada ya Kendi kudai kuwa tuzo hiyo ilipaswa kwenda kwa mkongwe wa dancehall, Redsan, akisisitiza kuwa ndiye anayestahili kutambuliwa zaidi katika tasnia kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa dancehall nchini Kenya na kimataifa