Entertainment

Chameleone Akanusha Kulipwa na Rais Museveni Kufamnyia Kampeini

Chameleone Akanusha Kulipwa na Rais Museveni Kufamnyia Kampeini

Msanii mkongwe kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone, amekanusha madai kwamba wasanii wanaomuunga mkono Rais Yoweri Kaguta Museveni wanalipwa fedha nyingi.

Akizungumza na kituo cha televisheni nchini humo, Chameleone ambaye yuko kwenye kampeni ya kumpigia upatu Museveni pamoja na wasanii wenzake Bebe Cool na Eddy Kenzo, amesema kuwa anafanya hivyo kwa hiari yake kama ishara ya shukrani na uaminifu kwa Rais Museveni.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Jamila, amefafanua kuwa hajalipwa kufanya kampeni hizo, bali ni kitendo cha kujitolea kwa sababu Rais alimsaidia alipokuwa mgonjwa mara kadhaa, na hivyo anaona ni wakati wake wa kurudisha wema huo.

Chameleone pia amesisitiza kuwa uungwaji mkono wake hauhusiani na maslahi binafsi pekee, bali unatokana na kutambua mchango wa Rais Museveni katika kudumisha amani na utulivu nchini Uganda.

Kwa sasa, msanii huyo anaungana na wasanii wengine wanaomuunga mkono mgombea wa chama tawala cha NRM Yoweri Museveni, wakishiriki katika mikutano na matamasha ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Januari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *