Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva na hitmaker wa ngoma Msumari, Diamond Platnumz, ameweka historia mpya baada ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kufikisha wafuasi milioni 1 kwenye mtandao wa Audiomack.
Takwimu hizo zinaonesha ukuaji mkubwa wa ushawishi wake kwenye majukwaa ya kidijitali, ikithibitisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika.
Audiomack, ambayo ni moja ya majukwaa makubwa ya kusikiliza muziki duniani, imekuwa chachu muhimu kwa wasanii wa Kiafrika kufikia mashabiki kimataifa.
Kupitia mafanikio haya, Diamond Platnumz ameendeleza rekodi yake ya kuwa kinara wa mitandao mbalimbali ya muziki kama YouTube, Boomplay, Spotify na Apple Music, ambapo nyimbo zake zimeendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.
Mashabiki wake wamempongeza kwa mafanikio hayo, wakimtaja kama mfano wa kuigwa katika kukuza muziki wa Afrika Mashariki kimataifa