Kampuni ya Facebook imetangaza rasmi kuwa itafunga app yake ya Facebook Messenger kuanzia mwezi April mwaka huu.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, mabadiliko hayo yataanza kwa watumiaji wa kompyuta za Mac na Windows. Baadaye, kampuni hiyo inapanga kuondoa kabisa Messenger kama app inayojitegemea na kubakiza huduma ya ujumbe ndani ya Facebook pekee katika majukwaa yote.
Messenger ilianzishwa mwaka 2008 kwa jina la Facebook Chat kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2011 na kuitwa Messenger. Tangu hapo imekuwa miongoni mwa majukwaa makubwa ya mawasiliano mtandaoni, ikitumika kutuma ujumbe wa maandishi, sauti pamoja na kupiga simu za video.
Facebook ilitumia Messenger kama sehemu ya mkakati wa ushindani dhidi ya majukwaa mengine ya mawasiliano kama WhatsApp, iMessage, WeChat na Skype.
Hatua hiyo ina maana kuwa watumiaji watalazimika kutumia Facebook moja kwa moja kwa huduma za ujumbe badala ya app tofauti ya Messenger.