Entertainment

Femi One Apokea Rasmi Tuzo ya Unkut Hiphop Awards 2025

Femi One Apokea Rasmi Tuzo ya Unkut Hiphop Awards 2025

Rapa nyota kutoka Kenya, Femi One, ametangaza rasmi kupokea tuzo yake ya Unkut Hiphop Awards 2025 katika kipengele cha Best Female Artist, hatua inayoendeleza rekodi yake kama mmoja wa marapa wa kike wenye ushawishi mkubwa katika Afrika Mashariki.

Kupitia ujumbe aliouweka mtandaoni, Femi One amewashukuru mashabiki wake kwa kura na upendo waliomuonyesha, pamoja na waandaaji wa tuzo hizo kwa kutambua mchango na juhudi zake kwenye muziki wa hiphop. Amesema tuzo hiyo ina maana kubwa kwake hasa katika mwaka ambao umetajwa kuwa wa mafanikio makubwa kwenye safari yake ya muziki.

Rapa huyo amesema mwaka 2025 umekuwa mwaka mkubwa kwa hip hop, akitaja mafanikio kama kushiriki kwenye Hennessy Cypher kama rapa mwanamke wa kwanza kuwahi kujumuishwa kwenye mradi huo mkubwa.

Femi One amesisitiza kuwa ataendelea kusukuma mipaka na kuvunja vizingiti ili kufungua njia kwa wasanii wa kizazi kijacho cha wasanii wa kike kwenye hiphop, akiahidi kazi bora zaidi na hatua kubwa katika safari yake ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *