Entertainment

Geoffrey Lutaaya Ashindwa Kiti cha Ubunge Kakuuto Kupitia NUP

Geoffrey Lutaaya Ashindwa Kiti cha Ubunge Kakuuto Kupitia NUP

Mgombea wa chama cha National Unity Platform (NUP), Geoffrey Lutaaya, ameshindwa katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Kaunti ya Kakuuto wilayani Kyotera, baada ya kupoteza dhidi ya mgombea wa chama tawala cha NRM, Ismail Lubega.

Lutaaya, ambaye alikuwa anawania kutetea kiti hicho, aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2021 baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha NUP katika Bunge la 11 la Uganda.

Hata hivyo, safari yake ya kisiasa imepata pigo kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi, ambapo Lubega wa NRM ameibuka mshindi.

Geoffrey Lutaaya anafahamika sana katika tasnia ya muziki nchini Uganda. Alipata umaarufu mkubwa mwishoni mwa miaka ya 1990 akiwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa bendi maarufu Eagles Production, iliyotoa wasanii wakubwa na nyimbo zilizotikisa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *