Gossip

Lydia Jazmine Akanusha Kusaidiwa Kimaisha na Wanaume Matajiri

Lydia Jazmine Akanusha Kusaidiwa Kimaisha na Wanaume Matajiri

Staa wa muziki kutoka Uganda, Lydia Jazmine, amekanusha vikali uvumi unaoenea mitandaoni ukidai kuwa amekuwa akipata ufadhili wa kifedha kutoka kwa wanaume maarufu ili kufanikisha maisha yake ya kifahari.

Akipiga stori na Youtuber mmoja nchini humo, mwimbaji huyo wa ngoma ya “Masukka” amesema kuwa hana mwanaume anayemgharamia maisha yake, akisisitiza kuwa kila kitu alicho nacho kimetokana na juhudi zake binafsi kupitia kazi yake ya muziki.

Mrembo huyo, amesema watu wengi wamekuwa wakidhania kuwa anasaidiwa na wanaume kutokana na mtindo wake wa maisha, lakini ukweli ni kwamba yeye anajituma na kujipatia kipato chake halali.

Lydia Jazmine ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao mara kwa mara wamehusishwa kimapenzi na wanaume mbalimbali katika tasnia ya muziki nchini Uganda, ingawa amekuwa akikanusha madai hayo kila mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *