Gossip

Msanii Akothee akerwa na shinikizo la mitandao kwa familia yake

Msanii Akothee akerwa na shinikizo la mitandao kwa familia yake

Mwanamuziki kutoka Kenya Akothee amewataka walimwengu kuacha kufuatilia na kuwawekea watoto wake viwango vya juu vya maisha, baada ya kuzuka kwa madai kuwa wanaishi maisha ya kuigiza mtandaoni.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Akothee ameonyesha kukerwa na watu wanaojaribu kuwawekea watoto wake viwango vya maisha vinavyodhaniwa kuendana na uwezo wake kifedha. Amesisitiza kuwa watoto wake wamelelewa katika maisha ya kawaida na hana mpango wa kuwalazimisha kuishi maisha ya kifahari kwa ajili ya kufurahisha mitandao ya kijamii.

Aidha, amewataka wanablogu kuwa makini na aina ya maudhui wanayoyapa uzito, akisema si busara kuzingatia maoni ya watu wasio na uzoefu wa kusafiri au kufahamu maisha ya mataifa mengine ulimwengu.

Kauli ya Akothee imekuja baada ya kuzua mjadala mtandaoni kufuatia tukio ambalo mwanamke mmoja alidaiwa kulazimisha binti yake kupiga picha pamoja naye, kisha picha hizo kusambazwa mitandaoni wakidaiwa walionekana wakinunua bidhaa katika maduka ya hadhi nchini Uingereza, licha ya mama huyo kujitambulisha kama tajiri mkubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *