Msanii na bosi wa lebo ya Next Level Music, Rayvanny, ametangaza rasmi mipango ya kumrudisha msanii wake Mac Voice ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya kimuziki.
Kupitia maelezo yake, Rayvanny amesema maandalizi ya kurejea kwa Mac Voice yako katika hatua za mwisho, akiwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kupokea kazi mpya kutoka kwa msanii huyo muda wowote kuanzia sasa.
Mbali na mpango wa kumrudisha Mac Voice, Rayvanny pia amefichua kuwa Next Level Music ipo mbioni kumtambulisha msanii mpya.
Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa lebo hiyo kuendelea kukuza vipaji vipya, kupanua wigo wa muziki wake na kuimarisha nafasi yake katika soko la muziki Afrika Mashariki.