Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, ameendelea kupanua wigo wa uwekezaji wake baada ya kutambulisha rasmi biashara yake mpya ya real estate.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy amewashirikisha mashabiki video ikionyesha nyumba zake za kifahari alizozipa jina la Naya Homes, ambazo zipo katika hatua za mwanzo ya ujenzi.
Hatua hii inakuja baada ya Nandy kufanikiwa kujijenga katika biashara ya muziki, ambapo ameendelea kutoa nyimbo zilizopata mafanikio makubwa, pamoja na kuingia na kushamiri katika biashara ya bidhaa za urembo.
Nandy anaendelea kuthibitisha kuwa mafanikio ya muziki yanaweza kuwa daraja la kufungua fursa nyingine za kibiashara, huku akiwahamasisha wasanii na vijana wengi kuwekeza na kujiandaa kwa maisha ya baadaye.
Sasa, kuwekeza kwenye sekta ya mali isiyohamishika kunatajwa kuwa hatua nyingine muhimu katika safari yake ya kujijenga kiuchumi.