Mtangazaji na mchekeshaji, Oga Obinna, amefunguka kuhusu matumizi makubwa aliyowahi kufanya katika mahusiano yake ya kimapenzi, akieleza namna alivyowahi kusaidia wapenzi wake wa zamani kifedha.
Kwa mujibu wa Obinna, aliwahi kumpa ex wake kiasi cha Shiliingi millioni 1.8 za Kenya ili kusaidia kulipia mkopo wa gari. Amesema msaada huo aliutoa kwa moyo wa dhati, bila kujua kuwa baadaye angekuja kuzungumziwa vibaya hadharani.
Mbali na hilo, Obinna amefichua kuwa katika mahusiano yake ya nyuma pia amewahi kununua magari kwa wapenzi wake wa zamani, akisisitiza kuwa alifanya hivyo kwa mapenzi na si kwa matarajio ya kulipwa au kushukuriwa.
Hata hivyo, Obinna amesema hajutii uamuzi wake, akisema alifanya hivyo kwa hiari na kwa moyo wa kusaidia, jambo linalompelekea kuzungumziwa vibaya mtandaoni.