Msanii nyota wa Bongo Fleva, Rayvanny, ameibuka kifua mbele akidai kuwa kwa sasa hakuna msanii anayemfikia, baada ya wimbo wake mpya “Toto” kufanikisha rekodi kubwa kwenye mtandao wa TikTok.
Wimbo huo umefanikiwa kufikisha jumla ya posti milioni 1 TikTok, hatua iliyomfanya kuwa msanii pekee kutoka Tanzania aliyefikia rekodi hiyo kwa mwaka huu.
Kupitia Instastory yake, Rayvanny hakusita kujitapa, akisisitiza kuwa hakuna msanii anayeweza kufikia idadi hiyo ya posti TikTok kwa mwaka 2025.
Hitmaker huyo wa Mama Tetema, ameongeza kuwa mafanikio hayo ni ya kipekee zaidi kutokana na ukweli kuwa wimbo huo ulitoka nje ya kipindi cha kawaida cha kutoa nyimbo.
Rayvanny pia amewashukuru mashabiki wake, hususan Gen Z, kwa sapoti kubwa waliyoonyesha tangu kuachiwa kwa wimbo huo.