Entertainment

Pia Pounds: “Naingiza mamilioni ya pesa mtandaoni kuliko matamasha ya klabuni

Pia Pounds: “Naingiza mamilioni ya pesa mtandaoni kuliko matamasha ya klabuni

Msanii wa muziki kutoka Uganda Pia Pounds amesema kuwa kwa sasa anaingiza fedha nyingi kupitia mapato ya muziki wake mtandaoni, akisisitiza kuwa majukwaa ya kidijitali yamekuwa chanzo kikubwa cha kipato kwa wasanii wengi.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Uganda, hitmaker huyo wa Tupaate alieleza kuwa yeye pamoja na menejimenti yake walifanya uamuzi wa kimkakati kubadili mfumo wa kusambaza muziki wao ili kuendana na mabadiliko ya soko la muziki.

Kwa mujibu wa Pia Pounds, waliamua kuacha njia ya zamani ya kusambaza muziki kwa njia za kawaida mitaani Kampala na badala yake wakaelekeza nguvu zao kwenye majukwaa ya kidijitali ambapo mashabiki wanaweza kusikiliza na kununua muziki wao kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Amesema hatua hiyo imeanza kuwaletea mafanikio makubwa kifedha, huku wakigundua kuwa mauzo na usikilizaji wa muziki mtandaoni yanaweza kuingiza mapato makubwa kuliko njia za zamani za usambazaji.

Kwa mujibu wake, ingawa baadhi ya wasanii bado wanategemea zaidi maonesho ya vilabuni na matamasha ili kupata kipato, ukweli ni kwamba fedha nyingi sasa zinapatikana kupitia huduma za kusikiliza muziki mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *