Entertainment

Pipi Jojo Afungua Akaunti Mpya ya YouTube Baada ya Mzozo na Chief Godlove

Pipi Jojo Afungua Akaunti Mpya ya YouTube Baada ya Mzozo na Chief Godlove

Msanii wa muziki, Pipi Jojo, ameanzisha akaunti mpya ya YouTube kufuatia mzozo na aliyekuwa bosi wake, Chief Godlove ambaye alimnyang’anya chaneli yake awali iliyokuwa na wafuasi zaidi ya laki moja baada ya kutofautiana kuhusu masuala ya mkataba.

Kupitia mitandao ya kijamii, Pipi Jojo amewaomba mashabiki wake kujiunga na chaneli yake mpya kwa kusubscribe, huku akiwahakikishia kuwa ataendelea kutoa kazi bora na za kuvutia.

Hatua hii imekuja baada ya kuvunjika kwa ushirikiano wake na Chief Godlove, ambaye alitaka amsainishe kwenye mkataba wa miaka 10, jambo ambalo Jojo alilikataa.

Mvutano huo umesababisha Pipi Jojo kupoteza chaneli yake ya zamani, lakini sasa ameanza upya na matarajio mapya. Mashabiki wake wanahimizwa kuunga mkono safari yake mpya ya muziki kupitia chaneli hiyo, huku tukio hili likionekana kama mwanzo wa ukurasa mpya katika maisha yake ya kisanii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *