Entertainment

Rayvanny Ajivunia Mafanikio ya Tamasha la Dubai

Rayvanny Ajivunia Mafanikio ya Tamasha la Dubai

Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny, ameendelea kuthibitisha umahiri wake baada ya kupiga show ya nguvu jijini Dubai, tukio lililohudhuriwa na maelfu ya mashabiki kutoka mataifa mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameonyesha furaha na kujivunia mafanikio hayo akisema kuwa mpaka sasa nchini Tanzania hakuna msanii mwenye onyesho kali kama alilolifanya juzi kati Dubai

Rayvanny ameongeza kuwa ngoma yake “Mama Tetema”, aliyomshirikisha nyota wa kimataifa Nora Fatehi, ndiyo wimbo bora zaidi Tanzania kwa mwaka huu, na hakuna msanii mwingine aliyetoa wimbo uliofikia kiwango hicho cha umaarufu.

Kauli hiyo imezua mjadala mtandaoni, baadhi ya mashabiki wakimtaja kama mmoja wa wasanii wachache wanaoendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa. Wengine wamesema Rayvanny amepiga hatua kubwa tangu alipotoka kwenye lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *