Akothee Amkingia Kifua Azziad Dhidi ya Wakosoaji wa Mitandaoni
Mwanamuziki, Akothee, amejitokeza kumtetea TikTok queen na mtangazaji Azziad Nasenya baada ya kuvamiwa mitandaoni kwa madai ya kuishi maisha ya kuigiza. Kupitia waraka wake Instagram, Akothee ameeleza kuwa anampenda na kumheshimu Azziad kwa kuwa na ndoto kubwa na kuonesha ujasiri wa kukimbizana na maisha. Amesisitiza kuwa hatua ya mrembo huyo kupata mkopo wa millioni 25 za Kenya na kununua nyumba akiwa na umri wa miaka 25 ni jambo la kupongezwa na si kulaumiwa, kwani ni nadra vijana kufanikisha mambo makubwa wakiwa na umri mdogo. Amesema kuwa wakati vijana wa rika la Azziad leo wanajitahidi kujenga maisha yao, wengi wa kizazi kilichomtangulia walihangaika na changamoto kubwa kama ndoa zilizoshindikana, kulea watoto peke yao na hata kutokuwa na akaunti ya benki wala ajira. Kwa maoni yake, hatua ya Azziad kuwekeza katika nyumba ni mfano bora wa kuchukua jukumu la maisha yake mapema. Akothee pia amekosoa wanaume wanaoendelea kumsema vibaya Azziad mitandaoni ilhali wao bado wanashindwa hata kumudu mikopo midogo. Kwa mtazamo wake, badala ya kumkosoa, Wakenya kwa jumla wana nafasi ya kujifunza kutoka kwake. Hata hivyo amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa Azziad ni msichana mwenye ndoto kubwa, anayeendelea kujijenga na kuwa chanzo cha msukumo kwa vijana wengi, na kwamba jamii inapaswa kusherehekea ujasiri wake badala ya kumshusha
Read More